OBvan ya pili barani Africa yakabidhiwa TBC toka China




Serikali ya CHINA imekabidhi msaada wa gari la
kisasa la kurushia matangazo ya nje ya
televisheni kwa shirika la utangazaji Tanzania
TBC lenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni
SITA.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa gari hilo
jijini DSM Makamu wa Rais wa CHINA, LI
YUCHUAN amesema msaada huo unalenga
kudumisha uhusiano mwema kati ya nchi hizo
mbili.
Amesema serikali yake inaamini kuwa gari hilo
litatumika kuwaunganisha Wachina na
Watanzania kupitia vipindi mbalimbali katika
Nyanja za Uchumi, Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Utamaduni.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dokta FENELLA
MUKANGARA ameishukuru serikali ya CHINA kwa
msaada huo na kusema utasaidia kuboresha
matangazao ya Redio na Televisheni kwa Shirika
la Utangazaji TANZANIA- TBC.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TBC,
CLEMENT MSHANA amesema gari hilo la
matangazao ya nje ni la kisasa ambalo litasaidia
kuboresha matangazo, ikiwemo wakati wa Siku
kuu za kitaifa pamoja na michezo kama mpira wa
miguu.
Powered by Blogger.