Songea ni zaidi ya manispaa.
Tanzania inasifika kwa kuwa moja ya nchi kubwa si tu kwa eneo la makazi bali hata kwa rasilimali watu wanaopatikana katika nchi hii.Tanzania ikifuata mgawanyo wa kikoloni wa maeneo imejikuta ikigawa sehemu katika ngazi ya mikoa,wilaya,kata,tarafa,kitongoji,balozi na mwishowe kaya.
Katika makala ya siku ya Leo najikita zaidi katika moja ya manispaa kongwe hapa Tanzania ikibeba idadi ya watu isiyopungua laki 5.Jina Songea si geni miongoni mwa wasafiri wengi wa nyanda za juu kusini.Ni manispaa iliyoko karibu kabisa na nchi jirani ya msumbiji.Manispaa hii inayokuwa kwa kasi hivi karibuni kutokana na uvumbuzi wa madini(uranium) ina pewa hadhi stahiki kutokana na sifa na uwezo mbalimbali wa wakazi wake hasa ukizungumzia mambo ya kilimo cha asili.
Wanasongea walio wengi wanalima mazao ya nafaka kama mahindi,mtama,ulezi na soya.
Nikijikita kwenye mada yenyewe ya songea kuwa zaidi ya manispaa ninakuja na vigezo mbalimbali nikianza na umaarufu na ukongwe wa songea miongoni mwa mikoa jirani.Watu wengi wanaliheshimu jina chili hats kuzania kama ni mkoa badala ya wilaya.